Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwango cha Ramsdale chavutia makipa Tanzania

Rams Pic Data Kiwango cha Ramsdale chavutia makipa Tanzania

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BAADHI ya makipa wa Ligi Kuu Bara wanatamani ubora wa kipa wa Arsenal, Aaron Ramsdale (23) ambaye anasifiwa na mabeki kutokana na umahiri wake wa kuchomoa mishale ya mastraika.

Jambo hilo limewatamanisha makipa kutamani kukutana na washambuliaji wenye viwango bora watakaodhihirisha kazi zao wakavyokuwa wanazuia mashuti yao.

Kipa wa Polisi Tanzania, Metacha Mnata alisema ubora wa mchezaji haijalishi anacheza nafasi gani, anapofanya kitu cha ziada dunia inajua kuna mtu anayewapa burudani kama anavyozungumzwa Ramsdale.

“Natamani kukutana na mastraika hodari, nikipangua mashuti yao ndipo ubora wa kazi yangu unaonekana. Kila kazi inahitaji maarifa na mbinu, tofauti na zamani ambapo eneo la makipa halikuangaliwa kwa undani kama sasa,” alisema.

Kipa wa Ruvu Shooting, Mohamed Makaka ambaye mechi dhidi ya Yanga licha ya timu yake kupigwa mabao 3-1, aliokoa hatari nyingi, na kwa hili alisema: “Jambo hilo natamani nilifanye kwa bidii, ili washambuliaji wawe wanajiuliza mara mbilimbili kupata mafanikio nikiwa nimesimama golini.”

Naye kipa wa Mtibwa Sugar, Aboutwalibu Mshery: “Natamani kuonyesha utofauti niandike historia ya kuja kusimuliwa na vizazi vingine nyuma yangu.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz