Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kivumbi Namungo vs Yanga ni mechi ya heshima leo

Yanga Afrika Leo Kivumbi Namungo vs Yanga ni mechi ya heshima leo

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dakika za mwisho dhidi ya Tanzania Prisons, Yanga leo ina mtihani mwingine itakapoikabili Namungo katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utapigwa uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza kuelekea mchezo huo Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema baadhi ya wachezaji waliokosekana katika mchezo uliopita kutokana na adhabu pamoja na majeraha wamerejea kwenye mazoezi na anaamini watasaidia timu.

“Tunaamini hauktakuwa mchezo wenye nafasi nyingi lakini tutatumia nafasi tutakazopata ili kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho,”amesema Kaze.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 35 baada ya michezo 14 wakati Namungo ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 14.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo Singida Big Stars inashuka uwanja wa nyumbani, Liti mjini Singida kuivaa Coastal Union.

Singida Big Stars inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 27 baada ya michezo 14 wakati Coastal Union ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live