Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo wa Uingereza na Real Madrid ashinda tuzo ya Golden Boy

Kiungo Wa Uingereza Na Real Madrid Ashinda Tuzo Ya Golden Boy Kiungo wa Uingereza na Real Madrid ashinda tuzo ya Golden Boy

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Kiungo wa kimataifa wa Uingereza na Real Madrid, Jude Bellingham ameshinda tuzo ya Golden Boy 2023 - iliyotolewa kwa mchezaji bora wa chini ya miaka 21 katika ligi kuu za Ulaya.

Mshambuliaji wa Colombia na Real Madrid Linda Caicedo, 18, alishinda tuzo ya Golden Girl.

Bellingham, 20, alihama kutoka Borussia Dortmund hadi Real katika msimu wa joto na amefunga mabao 13 katika mechi 14 alizocheza.

Tuzo hii inakuja baada ya kutambuliwa kama mchezaji bora wa chini ya umri wa miaka 21 katika kandanda ya dunia katika sherehe ya Ballon d'Or mwezi Oktoba.

"Ningependa kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya safari yangu kuanzia Birmingham, Dortmund na sasa Madrid. Singeweza kufikia hatua hii bila wao," alisema.

Chanzo: Bbc