Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo aliyekipiga Iceland arejea Azam

Kiungo Azammm Klabu ya Azam imekamilisha usajili wa kiungo, Adolf Bitegeko

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Azam imekamilisha usajili wa kiungo, Adolf Bitegeko aliyekuwa anaichezea timu ya Volsungur IF ya nchini Iceland.

Nyota huyo aliyewahi kukichezea kikosi hicho akiwa akademi amerejea nchini baada ya mkataba wake kumalizika huku akiwa ni miongoni mwa majina yaliyoitwa na Kocha wa Stars, Adel Amrouche kwa ajili ya AFCON inayoendelea Ivory Coast ingawa hakupenya.

Usajili huo ni wa kwanza kwa wachezaji wazawa katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15 huku akiwa ni wa nne baada ya, Mohamed Mustafa kutoka Al-Merrikh, Yeison Fuentes (Leones FC) na mshambuliaji, Franklin Navarro kutokea Cortulua FC.

Mbali na kuichezea Volsungur IF ila timu nyingine alizochezea kiungo huyo ni KR Reykjavik na KeflavĂ­k IF zote za Iceland.

Chanzo: Mwanaspoti