Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Singida afichua siri ya kumpoteza Aziz KI

Aziz Ki Mks.jpeg Kiungo Singida afichua siri ya kumpoteza Aziz KI

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Singida Big Stars, Aziz Andambwile ameweka wazi siri kubwa ambayo imechangia kumfunika kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephen Aziz Ki ni kutomruhusu amiliki mpira.

Andambwile na Ki walikutana juzi kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Azam ambao Singida BS ilifungwa 1-0 bao lililowekwa wavuni na Fiston Mayele dakika ya 82.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Andambwile alisema maelekezo ambayo alikuwa amepewa ni kuhakikisha Ki hawi na uhuru wa kumiliki mpira kwani kama akiwa nao ni mzuri kwenye kupiga pasi za mwisho.

"Kikubwa ni kumnyima nafasi ya kupokea mipira ya kupeleka kwa washambuliaji wa Yanga kwa sababu yeye ndio kila kitu anapokuwa yupo na mpira pale mbele na nilifanikiwa;

"Mimi ni kiungo mkabaji na nilikuwa nahakikisha eneo langu linakuwa bora kwa hiyo ilikuwa lazima nikutane na Ki kwa kuwa alikuwa kwenye eneo la kushambulia la timu yake."

Kauli hiyo iliungwa mkono na kiungo mwenzake wa Singida BS, Yusuph Kagoma ambaye alisema;"Tulikuwa na ubora kutokana na maelekezo ya kocha lakini pia kujitoa mimi kama mchezaji mwenyewe kwa sababu nataka kuwa bora kila siku."

Katika mchezo huo kulikuwa na bato kubwa kwenye eneo la kiungo ndani ya dakika 90 za mchezo huo, ukiwa ni tofauti na michezo mingine ya Singida iliyopita.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: