Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Simba atibua mipango ya Robertinho Kwa Vipers

Robertinho Vipers Simba Kiungo Simba atibua mipango ya Robertinho Kwa Vipers

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wakijiandaa kurudiana na Vipers FC ya Uganda, kiungo mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis ametibua mipango na mbinu za kocha wake, Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

Kibu ni kati ya wachezaji waliocheza vizuri katika mchezo uliopita wakati Simba ikishinda 0-1 ugenini dhidi ya Vipers, huku nyota huyo akiwa kipenzi cha Kocha Robertinho.

Akizungumza nasi, Daktari wa Simba, Edwin Kagabo, amethibitisha kuwa kiungo huyo anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa siku saba baada ya kupata maumivu ya misuli katika mchezo dhidi ya Vipers.

Aliongeza kuwa, maumivu hayo yatamfanya Kibu aukose mchezo wa marudiano dhidi ya Vipers utakaochezwa Machi 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

“Kibu anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani siku saba kutokana na maumivu ya misuli aliyoyapata katika mchezo wetu dhidi ya Vipers.

“Kukosekana kwake kutamfanya kocha amtafute mbadala wake, licha ya kuwepo katika mipango yake katika mchezo huo,” alisema Kagabo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live