Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Simba Aipa Ubingwa Yanga

Yusuph Macho Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Yusuph Macho

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Yusuph Macho ‘Muso’ amefunguka kuwa kutokana na kiwango bora ambacho Yanga wamekionesha kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, timu hiyo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga iliifunga Simba bao 1-0 ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii, kuashiria kufunguliwa kwa msimu wa 2021/22.

“Yanga imefanya usajili mkubwa msimu huu ambao ni kama unakwenda kurekebisha makosa ambayo waliyafanya kwa misimu minne nyuma" amesema Muso

“Ukitazama sasa hivi kikosi chao unaona kimeimarika katika kila idara jambo ambalo linampa mwalimu wakati mzuri wa kufanya chaguzi kwenye kikosi chake.

“Ushindi dhidi ya Simba ni ishara tosha kwamba kuna kitu wanakitaka msimu huu, na kama hawatakuja kubadilika mbeleni wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu kutokana na aina ya wachezaji ambao wamewasajili.

“Aucho (Khalid), Mayele (Fiston), Makambo (Heritier) na Djuma Shabani ni miongoni mwa wachezaji ambao kama hawatakumbwa na upepo mbaya wana nafasi kubwa ya kuipa Yanga mafanikio msimu huu.

Chanzo: globalpublishers.co.tz