Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Ruvu aingia anga za West Armenia FC

Kungo Ruvu Kiungo Ruvu aingia anga za West Armenia FC

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya West Armenia inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Armenia imetuma ofa rasmi ya kuhitaji saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Maafande wa Ruvu Shooting, Abalkassim Suleiman.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo ililiambia Mwanaspoti wanahitaji saini ya nyota huyo baada ya mkataba wake na Ruvu Shooting iliyoshuka daraja msimu huu kumalizika.

"Mkataba aliopewa haukuangalia maslahi ya mchezaji wenyewe hivyo aliomba kurekebishiwa baadhi ya vitu kisha utumwe tena aungalie na akiridhika atasaini dili hilo jipya," kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Abalkassim akizungumzia suala hilo alisema ni kweli amefuatwa na viongozi wa timu hiyo ila makubaliano bado hayajafikia sehemu nzuri japo kuna matumaini makubwa ya kujiunga nao.

"Timu za Namungo, Tanzania Prisons na Geita Gold ni miongoni ambao wanahitaji saini yangu ingawa kwa sasa akili yangu kama mchezaji ni kuona natumia hii fursa ya kwenda nje ya nchi," alisema.

West Armenia ni mojawapo ya timu ambazo hivi karibuni iliingia mkataba wa ushirikiano na Simba ya Tanzania ambao unatoa fursa ya kuuziana wachezaji, maendeleo ya kiufundi na

Chanzo: Mwanaspoti