Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Real Madrid apewa makavu" Cheza mpira acha malalamiko"

CCCC Kiungo Real Madrid apewa makavu

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Bwana Mdogo Aurélien Tchouaméni kutoa maoni yake kuwa siku hizi kumekuwa na mechi nyingi zisizo na umuhimu ndani ya msimu mmoja hali inayosababisha wachezaji wengi kuchoka na kushindwa kucheza mpira kwa miaka mingi, Legend Jérôme Rothen amemjibu.

Anasema:

"Unataka mechi chache? Basi ulipwe pesa kidogo."

"Mimi huwa natetea wachezaji. lakini sasa kwa hili, bwana Mdogo nitampiga. Mchezaji jishughulishe na kazi yako, kuwa mzuri uwanjani, ujitunze na kujiandaa vizuri kwaajili ya mechi zako"

"Vijana wa sikuizi wanajifanya wakubwa, kuna mechi za karanga ambazo huwataki kucheza."

"Mlundikano huu wa mechi haujaanza leo ni sawa tu na miaka 20-30 iliyopita. Ukiangalia Uchovu anaozungumzia kwa kiasi kikubwa unatoka nje ya uwanja, kuna vitu ambavyo wanavifanya havina umuhimu na wanafanya kuwa ni muhimu."

"Leo hii wachezaji wengi wanatumia maisha yao kwenye mitandao ya kijamii, ni watu wa kutembelea sehemu za wazi na kuonekana kwenye matamasha mbali mbali"

"Wao ni kupanda ndege kwenda kuona mapambano ya MMA au sehemu mbali mbali za starehe kama baa nchini Uturuki."

"Katika hali kama hizi, lazima uchoke na lazima uone kazi yako ni ngumu"

"Waache Malalamiko, Wacheze Mpira"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live