Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Mtibwa kuvaa viatu vya Boban

Majogorooo Pic Data.png Kiungo Mtibwa kuvaa viatu vya Boban

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kiungo wa Mtibwa Sugar Baraka Gamba Majogoro ameweka wazi nia yake ya kutaka kuvaa viatu vya nyota wa zamani wa Simba, Yanga, Coastal Union, Mbeya City timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Star' na nyingine kibao Haruna Moshi 'Boban'.

Majogoro ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti  ambapo amemtaja Boban kuwa kioo chake katika soka na anapambana kutaka kuwa kama yeye ama zaidi.

"Boban ndiye mchezaji wangu bora wa muda wote, nmekuwa namuona akicheza na nimejifunza vingi kutoka kwake. Kila siku napambana na kujifua ili niwe kama yeye au zaidi na hata kama nisippcheza kama yeye ila nikiwa uwanjani najitahidi kufanya yaliyobora ili kumuenzi fundi yule wa mpira ambaye kwa sasa amestaafu kucheza," alisema Majogoro na Kuongeza:

"Watu wengi wanaombeza Boban unakuta sio watu wa soka, yule jamaa alikuwa na kipaji kikubwa hususani kucheza eneo la kiungo na nadhani ubora wangu wa sasa unachagizwa na baadhi ya maufundi niliyojifunza toka kwake," alisema.

Kiwango cha Majogoro kimezidi kumarika mara kwa mara kwa miaka ya hivi karibuni ambapo msimu huu amejiunga na Mtibwa akitokea Polisi Tanzania pia ni miongonio mwa wachezaji walioliwakilisha taifa wakiwa na  Taifa Stars mwishoni mwea mwaka jana kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani zilizofanyika nchini Cameroon na Stars kuishia kwenye hatua ya Makundi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz