Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Mbuni hatihati kuivaa FGA Talents

Kiungo Mbuni Kiungo Mbuni hatihati kuivaa FGA Talents

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Mbuni FC, Festo Masanja anaweza kuwa nje kwenye mechi ya Ligi ya Championship dhidi ya FGA Talents baada ya kupata majeraha ya enka.

Masanja alipata maumivu hayo kwenye mchezo wa Transit Camp FC ambayo ilipigwa Oktoba 29 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Morogoro na timu hizo kutoka suluhu.

Kukosekana kwa kiungo huyo ambaye amekuwa ni tegemeo kwa kocha Leonard Budeba na msaidizi wake Daniel Kirai inaweza kuwa ni pengo kubwa kwa Mbuni FC kwani katika mechi Nane za Ligi alizocheza ameiwezesha timu hiyo kuvuna pointi 14 huku akifunga magoli mawili.

Akiongea na Mwanaspoti Dokta wa Mbuni FC, Shaban Seif amesema kwa sasa nyota huyo anaendelea vizuri japo ajaanza mazoezi kikosi lakini anaamini mpaka siku ya mechi labda anaweza kucheza.

"Tulimtoa Damu na sasa anaendelea vizuri japo ajajiunga na timu ila naamini hivi karibuni kila kitu kitakuwa sawa," amesema Seif

Ameongeza kuwa mbali na Festo Masanja pia mlinzi wao Omary Omary ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria naye anaendelea vyema na muda wowote kutoka sasa ataanza mazoezi na wenzake.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya FGA Talents ambayo itapigwa Jumapili hii katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kocha msaidizi wa Mbuni FC, Daniel Kirai amesema wako vyema na mipango yao ni kubakisha pointi tatu nyumbani.

Amesema wanatambua ubora na madhaifu ya mpinzani wao hivyo wamejipanga kupambana nao na kushinda ili kusogea katika nafasi za juu kwenye msimamo ambayo itafanya kuendelea kubaki kwenye njia ya kuwania kupanda Ligi Kuu.

Mbuni FC inashika nafasi ya Sita kwenye msimamo kwa alama 15 baada ya mechi tisa, imeshinda Nne,sare Tatu na kupoteza mbili huku ikifunga mabao 15 na na kufungwa nane.

Chanzo: Mwanaspoti