Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Mbrazil: Nipo Tayari Kwa Kazi Simba

Fraga Apic Kiungo Mbrazil: Nipo Tayari Kwa Kazi Simba

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HATIMAYE uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa aliyewahi kuwa mchezaji wa timu hiyo, Gerson Fraga anarejea kikosini hapo kupitia usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, 2021 na kutarajiwa kufungwa Janauri 15, 2022.

Wakati Simba wakisema hivyo, mwenyewe ameibuka na kusema: “Nipo tayari.” Fraga mwenye uraia wa Brazil, amekuwa ni kipenzi cha mashabiki wa Simba mara baada ya kujiunga na timu hiyo mwaka 2019 kabla ya kuachwa msimu uliopita kutokana na majeraha ya muda mrefu.

Akizungumzia juu ya Fraga kurejea Simba, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, alisema: “Fraga ni mchezaji mzuri, anaweza kukukabia na wakati huo huo kwenda kufungia.

“Kuhusu kurejea tena ndani ya Simba inawezekana kwa kuwa aliwahi kucheza kwa mafanikio makubwa sana ndani ya Simba na kila mmoja anafahamu hilo.

“Hivyo tutampa nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha Simba, kama benchi la ufundi litaridhika na uwezo wake basi tutamsajili.

“Inakuwa ni ngumu kwa Fraga kusajiliwa moja kwa moja kutokana na kutoka katika majeraha ambayo yalimuweka nje kwa zaidi ya miezi sita jambo ambalo tumeona ni vema akachunguzwa kwanza tusije tukaingia mkenge.”

Wakati huohuo, taarifa zinasema kwamba, kiungo huyo anayeishi Porto Alegre nchini Brazil sehemu aliyozaliwa, tayari ameongeza program za mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi kabla ya kutua nchini kujiunga na Simba.

Mtoa taarifa huyo alisema kwamba: “Fraga anawasiliana na viongozi na juzi walimpa taarifa za kumrejesha kikosini kwa ajili ya kuja kuchukua nafasi ya Lwanga.

“Mara baada ya kupata taarifa hizo, haraka aliongeza program za mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi ili kuhakikisha anakuwa tayari kwa mapambano.

“Hivi sasa anafanya mazoezi ya gym na kuchezea mpira chini ya uangalizi wa kocha wake anayemsimamia ili kuhakikisha anakuwa fiti zaidi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live