Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Juventus afungiwa miezi saba

Nicolo Fagioli Kiungo wa Juventus, Nicolo Fagioli

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Juventus, Nicolo Fagioli amefungiwa miezi saba kutokana na kukiuka sheria za mchezo wa kamari nchini Italia. Nyota huyo alikuwa katika orodha ya mastaa wanaokabiliwa na skendo hiyo ikiwahusisha mastaa kutoka Ligi Kuu England, Sandro Tonali (Newcastle) na Nicolo Zaniolo wa Aston Villa.

Fagioli, 22, amekutwa na hatia baada ya kugundulika kufuatia uchunguzi na kupigwa adhabu ya kukaa nje ya uwanja kwa miezi saba.

Hata hivyo baba yake mzazi alimtupia lawama wakala wa mtoto wake alipodai kuwa alimshauri kiungo huyo akafanyiwe matibabu kwa sababu ameathirika na michezo ya kamari.

Taarifa ilitolewa na mwendesha mashtaka mkuu wa Italia iliripotiwa kuwa kiungo huyo amechukuliwa hatua hiyo pamoja na kulipa faini ya Pauni 11,000.

Pia atahudhuria matibabu maalumu ya kisaikolojia ambayo yatadumu kwa miezi mitano au sita. Wachezaji wenzake wengine wa timu ya taifa ya Italia, Tonali na Zaniolo watapewa adhabu endapo itabainika nao walibeti uchunguzi ukikamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live