Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Ghana matatani kisa jezi ya Suarez

Thomas Partey X Suarez.jpeg Kiungo Ghana matatani kisa jezi ya Suarez

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Timu ya Taifa ya Ghana Thomas Partey amejikuta matatani na Mashabiki wa Ghana na kuitwa "Msaliti" kwa kitendo chake cha kubadilisha na jezi na Mchezaji wa Uruguay, Luis Suarez baada ya mchezo wa jana.

Ghana wamecheza na Uruaguay mchezo wa mwisho kundi H kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Dunia na kupoteza kwa mabao 2-0, hivyo kushindwa kufuzu.

Baada ya mchezo, Partey alibadilishana jezi na Luis Suarez ambae anachukiwa na raia wa Ghana akionekana kama kikwazo kwa Timu ya Ghana kushindwa kufuzu kwa hatua ya nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika ya Kusini, baada ya Suarez kuzuia mpira uliokuwa unakwenda golini kwa mkono na kuwakosesha Ghana goli katika mchezo huo.

Ghana walipata penati na Suarez kupewa adhabu ya kadi nyekundu kwa tukio hilo lakini Nahodha wa Ghana wa wakati huo, Asamoh Gyan alikosa mkwaju huo na Ghana wakatolewa hatua ya matuta.

Hivyo mchezo wa jana ulikuwa wa kulipiza kisasi kwa Uruguay kwani kabla ya mchezo Suarez aliulizwa kama ataomba radhi kwa Ghana na Afrika kwa ujumla lakini aligoma na kudai hakuna baya alilofanya kwani aliadhibiwa na mwamuzi na Ghana wao wenyew walishindwa kutumia faida ya kupata penati.

Majibu hayo yalizidisha hasira kwa Waghana hivyo kitendo cha Kiubgo wao kubadilishana jezi na mchezaji huyo, wameona ni usaliti mkubwa kwao na taifa lao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live