Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Congo amaliza Mkataba, Vigogo wa Kariakoo wapanda dau

Miche Mika Kiungo wa DR. Congo, Miche Mika

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa DR. Congo, Miche Mika huenda mwanzoni mwa mwaka 2024 kwenye dirisha dogo la mwezi Januari ambalo litafunguliwa Desemba 15, akajiunga na moja ya timu za Kariakoo baada ya kumaliza kandarasi yake na FC LUPOPO ya Congo .

Najua Miche Mika yupo kwenye mazungumzo na Wababe wa Kariakoo Simba SC, Yanga SC kwa ajili ya kuona uwezekano wa kumsajili Kiungo huyo ambae atakuwa mchezaji huru mwezi Januari.

Kwa mujibu wa upande wa mchezaji, wameniambia wapo kwenye mazungumzo kwasasa, wamepata ofa moja ya timu kubwa Tanzania ila bado hawajafikia muafaka wa kile ambacho mchezaji anakihitaji.

"Tunazungumza, Tulipata ofa lakini tukakataa kwasababu haikuwa ofa ile tunayoitaka, Kwa hivyo bado tunazungumza."- amesem mmoja ya wasimamizi wa Mika Miche.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live