Juzi kama alikuwa anamuambia Kocha Gamondi kuwa sistahili kukaa benchini kama ambapo alimwambia kwa vitendo Kocha Nabi wakati anaingia Yanga, alimkuta Feisal, Aucho na Bangala lakini hapohapo akahitaji namba uwanjani kwa jihadi na akafanikiwa kumtesa Nabi na kumfanya Kocha atafute mbinu ya kucheza na Viungo wote 3.
Bangala alirudi kucheza kama beki wa kati na Aucho akatumika namba 6 huku Sure Boy akipewa majukumu ya namba 8 na akafanya vyema ndiyo maana Mechi na Club Africain alidhihirisha umma kuwa class is permanent.
Kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, aliingia akiwa kiungo pekee asilia na akafanya kazi Bora Sana wakati wote wa dk 90, kila mpira aliogusa uligeuka kuwa dhahabu, pasi nyingi zilitembea, pasi fupi zilipigwa na pasi ndefu zilitumwa kila angle ya uwanja na zote zilitii na kufika sehemu aliyotaka zifike.
Kipimo Cha pass zake kilikuwa thabiti na wapokeaji wa pass hawakupata shida Kwani pass zake zilikuwa hazina ubaya.
Alibalance timu na kuamua timu iondoke vipi kutoka nyuma kuelekea kwa mpinzani na alisaidia timu pindi Mtibwa walipotaka kwenda kumsalimia Diarra kwa kupitia eneo la Katikati.
Huyu kwangu naona ndiye mchezaji bora wa mechi, alikuwa katika kiwango bora, moja kati ya Viungo Bora nchini waliofanikiwa kuwa kwenye kiwango kilekile misimu 10+ mfululizo ni Sure Boy.
Msimu huu Gamondi atapasua Sana kichwa eneo la kiungo Aucho + Mauya + Sure Boy + Mudathir + Jonas Mkude + Sheikhan Ibrahim Khamis.