Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiufundi zaidi; Yanga vs Al Ahly

Aziz Ki Al Ahly Yanga.jpeg Kiufundi zaidi; Yanga vs Al Ahly

Sun, 3 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga SC hasa kipindi cha kwanza nafikiri kama waliwashangaza Al Ahly na muundo wao wakiwa na mali wanatemgeneza "BOX MIDFILED" kwenye muundo wa 3-2-2-3 (Job Bakari na Bacca nyuma) mbele yao Aucho na Maxi na mbele yao zaidi ni Pacome na Aziz Ki huku Mzize anasaidiwa na wingbacks wawili: Lomalisa / Kibabage na Yao.

Kwa nini hivi? Na iliwasaidia vipi Yanga hasa kipindi cha kwanza?

1: Kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye kiungo (Numerical Superiority) wanne dhidi ya watatu wa Al Ahly, maana yake Yanga walikuwa na nafasi kubwa ya kumiliki mpira

2: Kuwasogeza wachezaji wao wa viungo katika maeneo hatari mita 20 za mwisho (Pacome na Aziz) kwa kufanya hivyo inawapa faida gani?

3: Kuwa karibu na goli kufunga na kutengeneza nafasi lakini pia kuwarudisha nyuma viungo wawili wa chini wa Al Ahly kushuka chini zaid (Attia na Dieng) maana yake Aucho na Maxi wanakuwa huru wakiwa na mali

4:Sehemu ambazo Yanga walifanikiwa kipindi cha kwanza kwasababu wingbacks wao pamoja na Outside CBs wao (Job na Bacca) walikuwa wanazuia wingers wa Al Ahly

6: Ni muundo wao wa ulinzi wakiwa na mali wao (rest defense) mara zote wanakuwa watano nyuma kwahiyo hata counter attacks wanakabiliana nazo vizuri

Kipindi cha pili Al Ahly wali solve lile swali la Yanga , wakaanza kuwa na subira, wanapasiana upande kwa upande, huku wakiwa na wachezaji wengi pembeni (create overloads wide areas) kwanini?

1: Kumtoa Aucho na Maxi ndani ili kukabia pembeni 2: Kwa kufanya hivyo eneo la kati linaanza kuwa wazi kwa Afsha 3: Rahisi kwa Al Ahly ku switch mpira , kwasababu safari hii Job na Bacca walikuwa wanakabia ndani zaidi na wingbacks wao wanakuwa peke yao

Yanga kuanzia kama dakika ya 70 timu yao ilianza kumeguka (disconnect) Aziz na Mzize wanabaki juu peke yao na distance kutoka kwao mpaka mstari wa kiungo ni kubwa sana matokeo yake Al Ahly wakaanza kutawala mchezo

Hesabu nzuri kwa Gamondi mpango wa mechi ulilenga kwenye kutazama mpango wa mpinzani wake ambaye anauwezo mkubwa. Kwa Asilimia 90 uchaguzi wa kikosi cha Yanga ulikuwa sahihi.

Yanga na Al Ahly kwenye mipira ya corners imekuwa ningumu sana kuifanyia kuwa goli kipindi chakwanza Yanga walipata corner 6 na Al Ahly zamu Yao ikawa kipindi cha pili ikipiga 9 ila timu zote zilishindwa kufunga goli.

Al Ahly kipindi cha kwanza waliingia kwakuwaheshimu Yanga kwakuwasubiri wamiliki mpira wa fanye makosa kipindi chapili wakabadili shape yao wakaanza kufunguka kwa Kasi ili kutafuta goli.

Lomalisa alipoumia ikawa tatizo kwa upande wa Yanga alikuwa hatari kwenye safu ya beki ya Al Ahly hivyo kuumia kwake ikaifanya safu ya ulinzi na kiungo ya Al Ahly kupungua presha ya kukaba kwenye upande wakushoto.

Takwimu zinaonyesha Al Ahly wamemiliki mpira kwa 52% wakati Yanga wakimiliki kwa 48%, hawakuaachana sana hii inamaana kila timu ilicheza kimkakati na malengo.

Al Ahly kipindi cha pili ili faidika zaidi kwakufanya mashambulizi ya kasi kufika haraka kwenye bokis la Yanga likawafanya wale ma wing back wa Yanga kukosa uhuru wakupanda kama kipindi cha kwanza.

Yanga inamiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kufanya safu yake ya ulinzi kucheza zaidi kwenye dimba la kati.

NOTE 1. Diarra anafanya kazi ya golikipa kuonekana kama ni rahisi sana anadaka anajua kuanzisha mashambulizi yupo speed sana. Save ya Diarra kipindi cha pili

2. Rami Rabia umri wake na kazi anayo ifanya it's fantastic.

3. Hii back 3 ya Yanga kwenye ulinzi Bacca, Job, Mwamnyeto wale wawili wa pembeni Lomalisa na Yao kwenye kupanda mashambulizi ni wamoto.

4. Kuna huyu kiumbe anaitwa Pacome ni brain ya soka uwezi ubora ubunifu wewe mpe pasi mbovu anaifanya kuwa mali safi. Pacome kasimama kuhesabiwa pale alipohitajika what a strike

5. Bacca defending 6. Rabia kitasa 7. Ali MaĆ¢loul fullback ya boli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live