Klabu ya Kitayosce (Tabora United) imefungiwa kusajili dirisha hili la usajili mpaka itakapowalipa wachezaji wanaowadai.
Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya wachezaji husika kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hiyo.
Wachezaji watatu wa kigeni walifungua kesi FIFA wakipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu na kutolipwa.
Klabu hiyo ilitakiwa iwe imewalipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini haikutelekeza huku hizo.
Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeifungia kufanya uhamisho wa ndani.
TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo.