Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitayosce waiangushia lawama TFF

Kitayosce Tatzo Lao Kikosi cha Kitayosce kilichoanza dhidi ya Azam FC.

Sat, 19 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Kitayosce, Pendo Lema amesema walikwenda jijini Dar es Salaam na wachezaji (20) kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC.

Jana (Jumatano) asubuhi walikamilsha malipo yote ya vibali vya wachezaji wao wote (TFF) wakaambiwa mtandao unasumbua hivyo wasubiri majina ya wachezaji wao yaingizwe.

Pia, walilipa deni la wachezaji walioenda kushitaki FIFA kwa kuvunjiwa mikataba yao, hivyo zuio la usajili likaondolewa ikabaki kuingiza majina tu kwenye system.

Ameendelea kusema, baadae mchana wakapewa taarifa kuwa majina (8) ya wachezaji wao yameingizwa kwenye system wasubiri majina mengine.

Ameeleza kuwa, wachezaji hao (8) sio wa kikosi cha kwanza ni wale waliopanda daraja na timu kutokea Championship.

Mpaka muda wa mchezo unafika amesema majina yaliyokuwa kwenye system wanaoruhusiwa kucheza yalikuwa (8) tu hivyo ikabidi waende hivyohivyo uwanjani.

Majina yote ya wachezaji wao tayari yameingizwa kwenye system mpaka sasa, ameeleza kuwa jana usiku ndio walipewa taarifa kuwa majina yote yako verified.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live