Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitambi atoa siri alivyokwepa mtego wa Yanga

Denis Kitambi 1080x640 Kitambi atoa siri alivyokwepa mtego wa Yanga

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Geita Gold, Denis Kitambi amefichua siri iliyowabeba mbele ya Yanga iliyowafunga bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara, akitaja nidhamu ya kujilinda na kushambulia kwa hesabu ni moja ya vitu vilivyoipa changamoto Yanga ya Miguel Gamondi inayoonekana tishio kwa kuwa inatoa dozi ya mabao mengi.

Kitambi amekutana na Yanga mara mbili msimu huu, moja akiwa na Namungo FC na nyingine ni juzi, Alhamisi akiwa na Geita Gold na katika michezo yote, amepoteza kwa bao 1-0 na ndiye kocha pekee msimu huu aliyepona kwenye mtego wa kufungwa mabao mengi kwenye michezo miwili tofauti.

Kocha huyo mzawa alisema kwa ubora wa Yanga ilimbidi kuwa na mpango mbadala ambao kwanza ni kuwapa heshima yao maana ukisema upishane nao madhara yanaweza kuwa makubwa, hivyo nidhamu ya kujilinda na kushambulia kimkakati imemsaidia.

"Yanga ina wachezaji wengi wenye ubora mkubwa, hilo lipo wazi, ila tulijiandaa vizuri tukiwa na lengo la kufanya vizuri kwa sababu tunajua ubora wao upo katika maeneo gani, kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana kwetu, lakini cha pili tuliimarika na kupata nafasi tatu," alisema kocha huyo.

Kulingana na namna ambavyo anaendelea kukijenga kikosi chake, Kitambi anaamini wanaweza kufanya vizuri katika michezo yao ijayo ili kuwa mbali na hatari ya kushuka daraja.

Geita ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 21 kwenye msimamo wa ligi wenye timu 16, utofauti wao na timu za juu hadi nafasi ya 11 ni mabao tu.

Mchezo ujao, Geita itakuwa nyumbani kuikaribisha Mtibwa Sugar ambayo inaburuza mkia kwenye ligi ikiwa na pointi 16, mechi itakayopigwa baada ya ligi kurejea mapema Aprili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: