Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitambi anukia Namungo

Kitambi Pic Denis Kitambi

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa kocha wa Fountain Gate inayoshiriki Ligi ya Championship, Denis Kitambi yupo mbioni kujiunga na matajiri wa Kusini klabu ya Namungo FC.

Kocha huyo ametoka Dar es Salaam leo na baada ya kufika Ruangwa moja kwa moja ameenda hadi uwanja Majaliwa kuangalia mazoezi ya Namungo akiwa na katibu wa timu hiyo, Omar Kaaya.

Namungo inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga utakaochezwa Desemba 7 katika uwanja wa Majaliwa saa 1:00 usiku.

Bado Uongozi wa Namungo haujasema lolote juu ya kocha huyo kuhusu ujio wake.

Mwanaspoti lilipata nafasi ya kuingia uwanjani hapo kwa kuruhusiwa dakika za mwisho lilimshuhudia kitambi akizungumza na wachezaj wa timu hiyo.

Kitambi alichukua takribani dakika tatu akizungumza na wachezaji hao kisha wakafunga rasmi mazoezi yao.

Inaelezwa kocha huyo anaenda kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi akisaidiana na Shadrack Nsajigwa.

Mwanaspoti likiwa uwanjani hapo lilimshuhudia Nsajigwa na viongozi wa benchi la ufundi wengine bila kocha mkuu Hanoor Janza na alipotafutwa kwa njia ya mtandao wa Whatsapp kocha huyo amesema; "Nipo nyumbani Zambia mwanangu anaumwa."

Kitambi ni miongoni mwa makocha wazoefu na soka la Tanzania baada ya kufundisha timu za Simba na Azam kwa nyakati tofauti akiwa kama kocha msaidizi.

Kocha huyo pia ana uzoefu wa kufundisha nje baada ya kuinoa timu ya AFC Leopards ya nchini Kenya.

Chanzo: Mwanaspoti