Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitambi aisikilizia Geita Gold

WhatsApp Image Dennis Kitambi.jpeg Kocha Mkuu wa Geita Gold iliyoshuka kwenda Ligi ya Championship, Denis Kitambi

Sun, 2 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Geita Gold iliyoshuka kwenda Ligi ya Championship, Denis Kitambi amesema hatima yake itaamuliwa na bodi ya timu baada ya kufanya tathmini ya kumalizika msimu, huku akichomoa kueleza msimamo wake.

Geita imeshuka Ligi Kuu sambamba na Mtibwa Sugar baada ya kudumu kwa misimu mitatu ikimaliza nafasi ya 15, ikivuna pointi 25 kupitia mechi 30 na kushinda mitano, sare 10 na kupoteza 15.

Kitambi alisema hawezi kuweka wazi kama ataondoka ama atasalia ili aanze upya msimu ujao kwani hilo ni suala la viongozi baada ya kufanya tathmini.

“Hivyo hayo mengine ya tathmini ya nini kitatokea tutafanya baada ya mchezo wa mwisho ligi ikimalizika, lakini suala la usajili na matumizi ya nafasi za mabao naweza nikasema ndiyo vimechangia sisi kuwa katika wakati mgumu ambao tupo sasa,” alisema kocha huyo wa zamani wa Azam, Simba na Namungo.

“Kuendelea ama kuondoka hayo ni mambo ya huko mbeleni kwanza kipaumbele chetu kilikuwa ni kuangalia namna ya kubaki Ligi Kuu katika mechi ya mwisho dhidi ya Azam lakini imeshindikana. Juu ya hatma yangu hilo ni suala la kusubiri, tutakaa chini na bodi kuamua kama wameridhishwa namoi au la.”

Awali, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Geita, Yefred Myenzi alinukuliwa akikiri benchi la ufundi la timu hiyo liliangushwa na usajili mbovu uliofanyika kutokidhi matarajio, huku akiahidi kuipambania timu isishuke daraja.

“Sisi kama halmashauri mpango wetu ni kuhakikisha tunatumia nafasi ya mechi zilizobaki angalau kupambana ili timu ibaki kwenye ligi ili ijipange vizuri kwenye usajili unaokuja, naamini tunaweza kufanikiwa na tukawapa furaha wananchi wa Geita,” alisema Myenzi

Chanzo: Mwanaspoti