Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitambi aanza na Yanga

Kocha Kambi.jpeg Denis Kitambi

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuijunga na klabu ya Namungo, kocha Denis Kitambi ameanza na majukumu ya kuisimamia timu hiyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga.

Kitambi alifika rasmi wilayani hapa Jumatatu jioni na moja kwa moja alienda kutazama mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yanafanyika usiku kwenye uwanja wa Majaliwa.

Kocha huyo ambaye ametambulishwa kama msaidizi, anasimama leo kwenye benchi huku akiwa ametazama mazoezi mara moja tu.

Kitambi akiwa uwanjani hapa kabla ya mchezo kuanza aliacha benchi la awali linaloongozwa na Shedrack Nsajigwa (Msaidizi) akisimamia mazoezi hayo.

Wakati Nsajigwa akisimamia mazoezi, Kitambi alikuwa anafatilia kila zoezi kwa ukaribu akiwa amekaa kwenye benchi.

Chanzo: Mwanaspoti