Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitabu cha Ajibu na ukurasa wa Chama Jangwani

Gamondi Chama Dube Abuya 91021 Kitabu cha Ajibu na ukurasa wa Chama Jangwani

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Ibrahim Ajibu anatoka Simba na kujiunga na Yanga Sc ni muda ambao Yanga ndio walikuwa wamedominate ligi yetu na Simba walikuwa wanapitia ukame wa makombe but Ajibu ndio alikuwa mchezaji tegemezi.

But mambo yakibadilika baada ya Ajibu kufika Yanga sababu Simba walitake over na kudominate ligi yetu kwa kuchukua makombe licha ya performance ya Ajibu kuwa nzuri lakini hakupata makombe na alitoka Simba ili kufata makombe Yanga badluck akapishana na gari la mshahara.

Jambo lilopelekea kupewa jina la Gundu na aliyekuwa Afisa habari wa Simba kwa wakati huo Haji Manara japo badae Ajibu alirejea Simba na kuweza kutwaa makombe ambayo aliyokosa japo wananchi walikuwa bado wanahitaji sana huduma yake kwa kiasi kikubwa.

Kuelekea msimu ujao Chama atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga akitokea Simba ambayo imepitia ukame wa makombe kwa miaka 3 huku Yanga wakiwa wamedominate kwa hiyo miaka yote sasa swali langu ni je Chama atasoma kitabu cha Ajibu au atakuja na jarada lake tofauti pale Jagwani.

Chama awe na performance kubwa ila Yanga wapoteze dominance yao, Chama awe na uwezo wa kawaida ila Yanga watwae makombe as normal au Chama awe na high performance na Yanga watwae makombe au Chama na Yanga wote waangukie pua.

Maswali haya yapo kurasa ya mwisho ya kutabu cha Ajibu Migomba sina majibu ila nasubiri kurasa mpya ya Chama Jagwani.

Tupende kuupa muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: