Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisubi Matumaini Yapo Simba

Kisubi Jeremiah Kisubi

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIPA wa Simba, Jeremiah Kisubi, amefunguka kuwa ana matumaini ya kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi hicho licha ya uwepo wa makipa wengine wazoefu akiwemo Aishi Manula na Beno Kakolanya.

Kisubi ni ingizo jipya ndani ya Simba ambapo amejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Prisons.

Kisubi alisema: “Simba ni klabu kubwa, ninayofuraha kujiunga na timu hii, matarajio yangu kwa sasa ni kuhakikisha napata nafasi ya kucheza.

“Natambua kuna makipa wengine hapa ambao ni wazoefu kama Manula na Kakolanya, lakini bado naamini nafasi yangu ipo.

“Naamini katika kupambana, hivyo nitapambana ili kuhakikisha ninamshawishi mwalimu ananipa nafasi ya kudaka kwani Simba itashiriki michuano mingi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live