Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisu ataja siri kuiua Yanga

Lenny Kisu.jpeg Beki wa Ihefu, Lenny Kisu

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Ihefu, Lenny Kisu ametengeneza rekodi yake dhidi ya Yanga baada ya kuifunga mabao ambayo yametibua rekodi mbili za timu hiyo ya wananchi katika misimu miwili mfululizo.

Yanga msimu uliopita ilienda kwenye Uwanja wa Highland Estate, Mbarali ikiwa haijapoteza mchezo katika mechi 49 mfululizo za Ligi Kuu Bara, Ihefu ikashinda 2-1 na kuivunja rekodi hiyo, Kissu akifunga bao la pili lililoipa timu yake pointi tatu.

Msimu huu Yanga ilidumu siku 73 katika mechi zake 7 kucheza bila kupoteza, Ihefu iliitibulia timu hiyo kwa kuifunga 2-1 juzi kwenye Uwanja wa Highland Estate huku Kissu akifunga bao la kwanza na kusawazisha.

Akizungumza na Mwanaspoti juu ya rekodi hiyo, Kisu alisema anajisikia furaha kuifunga Yanga kwa mara ya pili katika mabao muhimu.

"Kwa upande wangu naona ni furaha kufanya kitendo cha kujirudia dhidi ya timu kubwa kama Yanga, sio tu kuifunga bali ni mabao muhimu kwa timu yangu;

"Msimu uliopita nilifunga bao la pili ambalo lilifanya tupate pointi tatu na sasa nimefunga bao la kusawazisha na kuirejesha timu mchezoni, nafurahia muendelezo wangu."

Kisu alisema kutumia vyema nafasi zinazopatikana ni heshima kubwa kwa mchezaji na manufaa kwa timu.

"Kabla ya mchezo, usiku dokta alikuja chumbani na kuniambia anaona kama nitafunga tena, nilimwambia nikipata nafasi nitafunga na ndio maana katika mchezo baada ya kufunga nilimfuata,"

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: