Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kissu aoga noti kisa Yanga

Leny Kisu Kisu Lenny Kissu

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Lenny Kissu ni jina tishio kwa Djigui Diarra hii ni kutokana na kumvunjia rekodi kwenye misimu miwili mfululizo.

Alianza msimu uliopita akiipa Ihefu FC pointi tatu muhimu kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Highland Estate baada ya kufunga bao la pili kwenye ushindi wa mabao 2-1 na kuitibulia Yanga rekodi ya kushindwa kumaliza msimu bila kufungwa baada ya kucheza mechi ya 49 kwenye mechi za ligi kuu.

Oktoba 4 mwaka huu, Kissu akamtibulia tena rekodi Diarra ambaye kwenye mechi tatu kabla ya kuvaana na Ihefu alikuwa hajaruhusu nyavu zake kutikiswa Yanga ikikubali kichapo cha mabao 2-1.

Mwanaspoti limefanya mahojiano na nyota huyo beki kisiki wa Ihefu FC na kufunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna alivyovuna fedha baada ya kuitungua Yanga misimu miwili mfululizo.

AOGA NOTI KISA YANGA

Ni nadra sana mchezaji mmoja kufanya maajabu kwa timu za Simba na Yanga mara mbili mfululizo lakini kwa Kissu ni kawaida kama anavyothibitisha mwenyewe.

“Kujiamini na kuamini katika upambanaji ndio siri ya mafanikio yangu, kuifunga Yanga sio rahisi ila ni sehemu ya kuamini katika kufanya kile ambacho kinaweza kuleta matokeo mazuri;

“Nimepata nafasi ya kuwafunga Yanga mara mbili mfululizo hii ni kutokana na kupambana na kuamini kiuwa hakuna kinachoshindikana pia kuaminiwa na kocha kwa kunipa nafasi ya kucheza.” anasema.

Kissu anasema licha ya sifa kubwa alizopata baada ya kuifunga Yanga misimu miwili mfululizo anakiri kuwa amepata zawadi nyingi za pongezi kutoka kwa viongozi na mashabiki wa timu hiyo.

“Kwenye kila zawadi yoyote fedha ni lazima na imekuwa ikiambatana na kitu kingine sitaki kuweka wazi ni vitu gani na kiasi gani cha fedha nimepata kwa sababu zawadi sio matangazo, ila ninachoweza kusema ni ndani ya misimu yote miwili nimenufaika kutokana na kuifunga timu hiyo,” anasema.

AWEKA REKODI

Kuifunga Yanga ni rekodi kwa mastaa wanaocheza timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, hilo limethibitishwa na Kissu ambaye amekiri ameweka rekodi mbili mfululizo.

“Mabao niliyoifunga Yanga kwa misimu miwili mfululizo yanaingia kwenye historia ya mabao niliyofunga kwenye maisha yangu ya soka. Nimeifunga Yanga ambayo ilikuwa haijaruhusu bao na bao langu ndo la kwanza kufungua nyavu zao msimu uliopita na kukata ngebe zao.”

“Msimu huu pia nimetibua rekodi ya kutokufungwa nilipofunga bao la kusawazisha,” anasema Kissu.

KUIFUNGA YANGA PITA HUMU

Anafunguka ili kuzifunga Yanga na Simba lazima ujiandae vizuri kisaikolojia na maandalizi mengine ya mechi.

“Kukutana na Simba, Yanga kunakuwa na maandalizi ya tofauti na ukikutana na timu nyingine. Hata hivyo, mimi binafsi nina maandalizi yangu tofauti.”

“Benchi la ufundi na viongozi kukiwa na mechi na timu hizo huwa wanaungana na kutuweka pamoja wachezaji, hili pia linachangia sisi kama wachezaji kujiweka katika hali ya tofauti, kupumzisha miili yetu kwa wakati, tukiamini kuna mchezo mgumu na muhimu mbele, hii inaweza kuwa siri ya mafanikio,” anasema.

KUTOKA KIPA HADI BEKI

Kila mchezaji ana historia yake kwenye maisha ya soka kuna walio zaliwa na kipaji cha kucheza na ambao wanaupenda mchezo huo na kufundishwa kwa upande wa Kissu anakiri amezaliwa kucheza soka na alianza kuchza eneo la kipa kabla ya beki.

“Kwenye makuzi yangu ya soka sikuwa beki nilianza kujifunza soka au kufundishwa nikiwa nacheza nafasi ya kipa kabla sijahamia nafasi za ndani;

“Wazazi wangu baadae ndio waliamua kunichagulia nafasi ya kucheza na walitaka nicheze eneo la ulinzi (Beki) nafasi ambayo nacheza hadi sasa na sikuwahi kuambiwa sababu ya wao kutaka mimi nicheze eneo hilo,” anasema.

Kissu anasema haikumpa wakati mgumu kubadili nafasi hiyo, kwani alifanyiwa mabadiliko hayo akiwa na umri mdogo hivyo ilikuwa ni rahisi kwake kubadilika na kuzoea nafasi mpya.

NYOSSO DARASA TOSHA

Kwenye maisha kila mwanadamu amekuwa na kitu anajifunza kwa aliye mtangulia na aliyemfanya apende kufanya anachokifanya kwa wakati huo kama ilivyo kwa Kissu.

“Kuna mabeki wengi wazuri wanaocheza nafasi yangu lakini kioo changu ni Juma Nyosso kwani nimekuwa nikimtazama na kujifunza vitu vingi kutoka kwake tangu nimeanza kucheza nafasi hii;

“Najisikia furaha kupata nafasi ya kucheza naye timu moja nazidi kuwa bora na nilishamtamkia ni mimi mwanafunzi wake, nimekuwa nikijifunza vitu kutoka kwake, hivyo amekuwa mwepesi wa kunielewesha,” anasema.

34, 16 NAMBA ZENYE MAANA

Kila mwanadamu ana namba zake za kumbukumbu nzuri na mbaya kwenye maisha yake kama ilivyo kwa Kissu na ametaja namba mbili ambazo ameweka wazi kuwa ni namba zenye maana nzuri kwake.

“34 ni idadi ya mechi nilizocheza nikiwa na timu yangu ya Ihefu FC, ni rekodi nzuri kwangu kwani ni timu ambayo imenifanya nicheze misimu miwili mfululizo kwa ubora na naamini nitakuwa bora hadi msimu unamalizika;

“16 ni namba ya jezi yangu ambayo nimekuwa nikiivaa na imekuwa na maana kubwa sana kwangu kwani ni tarehe ambayo familia yetu yenye watoto watano mimi nikiwa wa nne wengi tumezaliwa tarehe hiyo,” anasema Kissu ambaye alianza kukipiga Polisi Moro kwa msimu moja na baadaye Biashara United aliyoitumikia kwa misimu mitano na sasa Ihefu msimu wa pili.

Chanzo: Mwanaspoti