Kiungo msambuliaji wa Yanga, Tuisila Kisinda raia wa Congo DR ni ruksa kuwavaa AL Hilal ya Sudan katika mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho Jumamosi, Oktoba 8, 2022 katika Dimba la Mkapa.
Hayo yamesemwa na uongozi wa Yanga kufuatia taarifa mbalimbali kusambaa mitandaoni zikidai kuwa Kisinda haruhusiwi kucheza mchezo huo kwa madai kuwa usajili wake ulichelewa.
Yanga imesema kuwa Kisinda anaruhusiwa kucheza kutokana na kwamba CAF walifungua dirisha tena la usajili ambapo Yanga walimwongeza Kisinda na kumtoa Kambole, hivyo jina la Kisinda lilipata nafasi ya kuingizwa kwenye mfumo wa CAF kwa wakati.