Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisiki Azam aweka mkwanja mzito kupata njumu

Njumu Pic Data Kisiki Azam aweka mkwanja mzito kupata njumu

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI kisiki wa Azam FC, Yakub Mohamed ameonyesha kupenda kazi yake baada ya kuamua kuwekeza katika vifaa anavyotumia pindi anapokuwa yupo uwanjani.

Yakub ni kati ya wachezaji wanaokuwa wanawaka pindi wanapokuwa uwanjani, kuanzia kichwani akiwa na mtindo wa kuweka nywele zake rasta mpaka katika kiatu anachovaa mguuni.

Mwanaspoti lilizungumza nae juu ya kiatu anachokivaa, aliweka wazi kwamba yeye huwa anaagiza viatu vyake kutoka nchini Afrika Kusini au Uturuki.

"Ndio mimi huwa naagiza kutoka nje, nanunua viatu hivi kwa Dola 300, napendelea kutumia Nike Mercury au Nike Tempo na ninajisikia vizuri".

Thamani ya kiatu hiko kwa pesa za kitanzania ni zaidi ya Sh 600,000 lakini Yakub ameweka ikiwa ni kuhakikisha kazi yake inaenda kama alivyopanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz