Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa penalti, Jonesia apewa shavu

Jonesia Rukyaaa Mwamuzi Jonesia Rukyaa

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mwamuzi wa zamani Methew Akram amewataka wadau wa soka kuheshimu uamuzi wa mwamuzi wa fainali ya Simba dhidi ya Yanga, Jonesia Rukya kwa madai alijitahidi kuumudu mchezo.

Juzi ilikuwa fainali ya kibabe ya Ngao ya Jamii iliyowakutanisha watani hao katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga na kushuhudia mikwaju ya penati 3-1 zikimpa Simba ushindi.

Akram aliliambia Mwanaspoti anashangaa kuona mitandaoni hadi wanahabari wanamlaumu mwanamama huyo wakati alijitahidi kuumudu mchezo kutokana na ushindani uliokuwepo.

“Yale mabao wafungaji walikuwa wameotea, tatizo wachezaji wa Yanga walishindwa kuzitazama hizo na walijua makosa yao mpaka mabao yakakataliwa.

“Mwamuzi alijitahidi sana kutunza presha ya wachezaji na mashabiki, wanasema kipa wa Simba alitoka katika mstari jamani wanaosema wengi wanaangalia marudio kwenye mitandao.

“Timu ikifungwa watu wanaanza kutafuta sababu lakini wakumbuke wakati penalti zinapigwa mwamuzi anatakiwa kumuangalia mpigaji na kipa kwa wakati mmoja, sasa kama macho yalikuwa kwa mpigaji na sio kwa kipa au kwa kipa na sio kwa mpigaji wasimlaumu,” alisema Akram.

Akram alisema Jonesia alijitahidi kutafsri sheria 17 licha ya kuchezwa kwa faulo nyingi hasa kipindi cha kwanza lakini alijitahidi hata kutoa kadi aliamua kuacha ila angekuwa mwamuzi mwingine kadi zingemwagwa nyingi mpaka mchezo ungevurugika.

Katika hatua nyingine Akram aliwataka waamuzi wote wanaopewa dhamana ya kushika filimbi katika Ligi Kuu Tanzania Bara kutenda haki na kuzitafsiri vyema sheria ili kila timu ipate inachostahili kutokana na uwekezaji mkubwa ambao zimefanya.

Chanzo: Mwanaspoti