Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa mvua AFCON 2023 yasogezwa 2024

B51E017E 11DC 4383 B340 1A55CAEF5E18.jpeg Kisa mvua AFCON 2023 yasogezwa 2024

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zilizotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ivory Coast zimeahirishwa rasmi na kupangwa kufanyika Januari 2024 nchini Ivory Coast.

Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika CAF, Patrice Motsepe amethibitisha hilo akitaja sababu kuu ya kusogezwa mbele kwa mashindano hayo ni kutokana na mvua kubwa zinazoweza kunyesha Juni-Julai, 2023.

Kamati ya Utendaji ya CAF imekutana Rabat, Morocco leo imefikia makubaliano ya kurejesha fainali ya Ligi ya Mabingwa kucheza kwa mfumo wa nyumbani na ugenini huku pia michuano ya Super Cup ikitarajiwa kutimua vumbi Agosti 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live