Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said, amesema wamemboreshea maslahi straika wao Fiston Mayele ili aendelee kuwatumkiwa Wananchi.
Eng. Hersi ameyasema hayo jana alipokuwa akifanya mahojiano na Clouds FM ambapo alifungua masuala mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo anayoiongoza.
"Tuisila Yanga ilimuuza kwenda Berkane na tulipata pesa nyingi na sio pesa tu, tulipata Pre Season Morocco kama sehemu ya Deal, wakati tunamtoa tulimleta Moloko, football ipo hivyo kuna wakati unahitaji kufungua milango Mtu aende lakini kuna saa huwezi kuruhusu Mchezaji mzuri aondoke.
"Mayele ofa kadhaa zimekuja hatujamzuia kwa maana Mchezaji aondoke lakini tumeboresha mahitaji yake ili awe huru kubaki," alisema Eng. Hersi.