Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa kuikataa Man United, De Jong ageuka dili Barcelona

De Jong Frankoe.jpeg Kiungo wa Barcelona Frankie De Jong

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa klabu ya Barcelona Frenkie De Jong na timu ya taifa ya Uholanzi Frenkie De Jong amegeuka kua lulu ndani ya klabu ya Barcelona baada ya kuikataa klabu ya Manchester United katika dirisha kubwa lililopita.

Frenkie De Jong amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Barcelona chini ya kocha Xavi Hernandez tangu tu alipoikataa klabu ya Manchester United kwenye dirisha la usajili lililopita, Hii imemfanya mchezaji huyo kuimbwa sana ndani ya klabu hiyo.

Kocha Xavi Hernandez amenukuliw akimmwagia sifa kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi na hiyo ni kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu hiyo, Kiasi kwamba kocha Xavi amevutiwa nae sana tofauti na msimu ambao umemalizika.

Taarifa zilieleza mwanzoni kocha Xavi alipoingia ndani ya klabu ya Barcelona moja ya wachezaji ambao hawakua kipaumbele chake basi ni Frenkie De Jong, Lakini baada ya kugoma kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliomalizika amegeuka kua mchezaji muhimu zaidi kwenye kikosi cha Barca.

Frenkie De Jong leo atakua moja ya wachezaji ambao watakua wanaiongoza klabu ya Barcelona dhidi ya Manchester United katika dimba la Old Trafford kwenye mcherzo wa kombe la Uefa Europe League, Ikiwa ni uwanja ambao alihitajika zaidi kuucheza kama uwanja wake wa nyumbani alikataa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live