Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Yanga, Asukile afungiwa

Asukile Pic Data Kisa Yanga, Asukile afungiwa

Wed, 12 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungia michezo mitano na faini ya Sh 500,000 mchezaji wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile.

Hatua hiyo imekuja baada ya kamati ya mashindano kupitia ripoti za kombe hilo na ikajiridhisha kuwa Asukile ametenda makosa ya kutoa maneno ya kejeli, kashfa, udhalilishaji na shutuma dhidi ya timu pinzani  (Yanga), wachezaji wa kigeni wa klabu hiyo pamoja na mwamuzi wa mchezo na TFF.

Kufuatia makosa hayo TFF imemfungia kucheza michezo mitano ya mashindano rasmi ya TFF na faini ya shilingi 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 38:2, 39:5-3 ya kanuni ya Ligi Kuu ambazo zinazosomeka pamoja na kanuni za kombe la Shirikisho.

Pia kamati kupitia ripoti za mchezo ilibaini Asukile kutoa shutuma  za rushwa dhidi ya timu pinzani na shauri hilo limepelekwa katika kamati ya nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Ofisa habari wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo ilieleza zaidi kwa kuwaonya wachezaji, viongoiz na mashabiki kufuata utaratibu wa kanuni za mashindano wanayoshiriki.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz