Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Yanga, Ahamada achukia soka

Ali Ahamada.jpeg Ali Ahamada

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba moja wa Azam FC, Mcomoro, Ali Ahamada amesema anahitaji muda kuzoea Ligi Kuu Bara huku akikiri yeye ni bora lakini matokeo dhidi ya Yanga yalimfanya achukie soka.

Kipa huyo pamoja na kufanya vizuri kwenye baadhi ya michezo, amekuwa akilaumiwa kwa kufungwa mabao yanayooneka ni ya kizembe kwenye ligi hiyo.

Ahamada aliyewahi kucheza Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’ akiwa Toulouse, alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Azam FC mwanzoni mwa msimu huu, ameliambia Mwanaspoti  anapitia wakati mgumu kutokana na kucheza kwa mara ya kwanza soka la Afrika.

“Ni mapema sana kutokuaminiwa ndani ya timu yangu kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kucheza soka la Afrika, nahitaji muda ili niweze kufanya yale yanayotarajiwa na wengi,” alisema na kuongeza;

“Nafurahi kucheza soka la Tanzania, nimegundua ni nchi ambayo mashabiki wake wanapenda mpira lakini siyo wavumilivu timu inapopata matokeo mabaya, hili linanifanya niendelee kujifunza.”

Ahmada alisema anashukuru uongozi wa timu hiyo kwa kumwamini na kumpa nafasi ya kuitumikia timu hiyo na anaomba kuaminiwa zaidi ili kuwapa kile kilichowavutia na kumpa mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

Akizungumzia soka la Tanzania amezitaja Simba na Yanga zinapokutana ni mechi kubwa ambazo zinazungumzwa sana tofauti na mechi nyingine alizocheza hapa nchini.

“Dabi ya Simba na Azam, Yanga na Azam ni mechi ambazo zinazungumzwa sana na maandalizi yake yanakuwa tofauti na tunapokutana na timu nyingine hapa Tanzania,” alisema na kuongeza;

“Tulipata ushindi dhidi ya Simba hapakuwa na pongezi kutoka kwa mashabiki waliofurahia matokeo, ila baada ya kufungwa na Yanga ni siku ambayo niliuchukia mpira kwa sababu nilisikia maneno mengi na kubaini kuwa hii nchi haina uvumilivu kwenye matokeo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live