Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Urusi, Makamu wa Rais UEFA ang'atuka Madarakani

Skynews Karl Erik Nilsson Uefa 6306512 Karl-Erik Nilsson

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa UEFA amejiuzulu kwenye nafasi yake ya kuongoza michezo nchini Sweden baada ya kukosolewa baada ya Shirika la habari za Sky News kuweka wazi kuwa Kiongozi huyo alipiga kura kuitetea Urusi iondolewe marufuku ya kucheza soka Ulaya.

Karl-Erik Nilsson amekiri na kusema kuwa anaelewa imani juu yake haipo tena,hivyo ameamua kuachia ngazi kama mwenyekiti wa Shirikisho la soka la Sweden, takribani miezi minne tangu kushika nafasi hiyo.

Shirikisho la Michezo pamoja na Shirikisho la soka nchini Sweden yalikwishapinga timu za Urusi kuruhusiwa kuwemo kwenye mashindano ya Kimataifa tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live