Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Ubingwa, Mayele aionya Simba

Mayelee Pic Data Mayele aionya Simba

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSHAMBULIAJI kinara wa mabao ndani ya klabu ya Yanga mpaka sasa, Fiston Mayele amewaonya wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa msimu huu wakiwemo watani zao wa jadi Simba kuwa, wanataka pointi tatu za michezo iliyo mbele yao na wanauchukulia kila mchezo wao kama fainali.

Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa ambapo kabla ya ratiba ya michezo ya jana walikuwa wamefanikiwa kukusanya pointi 20 katika michezo nane ya kwanza, wakishinda mechi sita na kupata sare michezo miwili.

Jana Jumapili Yanga walitarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa, kwa ajili ya mchezo wa mzunguko wa tisa wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Mayele alisema: “Kama timu tunajivunia mwanzo mzuri wa msimu ambao tumekuwa nao ambapo mpaka sasa tunaongoza msimamo wa ligi, tunajua bado kuna kazi kubwa ya kufanya tuliyonayo katika adhima ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

“Kwa kutambua hilo tumejiwekea malengo ya kuhakikisha tunapambana kufa na kupona kwa kila mchezo ili kuibuka na ushindi huku tukiuchukulia kila mchezo kuwa ni fainali.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live