Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Taifa Stars, viporo zaidi vyanukia Ligi Kuu

77581 LIGI+PIC

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tatizo la viporo katika Ligi Kuu ya Bara linatarajiwa kuendelea kutingisha soka la Bongo baada ya timu ya taifa, Taifa Stars, kuomba muda zaidi wa kambi ya maandalizi ya kuing’oa Sudan ili kufuzu kwa fainali za Chan 2020.

Stars inatarajia kuanza kambi rasmi kwa ajili ya mchezo wa kufuzu wa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani Oktoba 6.

Kambi hiyo pia itakuwa kwa ajili ya wiki ya mechi za kimataifa za Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambayo itamalizikia Oktoba 12.

Stars na Sudan zinatarajiwa kurudiana Oktoba 18 nchini Uganda kutokana na sababu za kiusalama, hivyo kambi itakayoanza kabla ya Oktoba 6 iendelee hadi baada ya mechi hiyo ya Oktoba 18.

Habari za ndani zimesema bechi la ufundi la Stars chini ya kocha mkuu wa muda, Etienne Ndayiragije limependekeza kambi ya muda mrefu na hasa ukizingatia kuwa Sudan wamekuwa katika maandalizi ya muda mrefu.

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda alithibitisha kuwa wanahitaji kambi ambayo itawafanya kujiandaa vilivyo ili kushinda mechi dhidi ya Sudan.

Pia Soma

Advertisement
Mgunda alisema kuwa mkuu wa benchi la Ufundi wa Taifa Stars, Ndayiragije yupo na timu yake ya Azam na mpango uliopo ni kuita timu mchanganyiko kwa ajili ya wiki ya Fifa na wachezaji wa nje wakiondoka kambi iendelee kwa ajili ya michuano ya Chan.

“Ni kweli kuwa tunahitaji maandalizi ya muda mrefu kwa ajili ya mechi ya Chan dhidi ya Sudan. Tunahitaji ushindi wa mabao si chini ya mawili ili kufuzu makundi, hivyo kambi ya muda mrefu inahitajika.

“Ratiba inaonyesha kuwa wiki ya Fifa itaanza Oktoba 6 na kumalizikia 12. Mpango wetu ni kuita timu kwa ajili ya mechi za kirafiki za Fifa na michuano ya Chan kwa wachezaji wa ligi ya ndani,” alisema Mgunda.

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara tayari itaathiriwa na mechi hiyo ya Stars Chan ugenini Oktoba 18.

Mechi saba za Ligi Kuu zilizopangwa kuchezwa Oktoba 19 zinaweza kuathirika hasa kwa timu ambazo zinatakuwa na wachezaji watakaoitwa kwenye Stars kwa ajili ya michuano hiyo ya wachezaji wa ligi za ndani.

Chanzo: mwananchi.co.tz