Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Sure Boy, TFF yawaonya Azam

SURE BOY.png Wachezaji watatu wasimamishwa Azam FC

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Baada ya uongozi wa Azam FC, kuwasimamisha wachezaji wao, Aggrey Morris, Aboubakary Salum ‘Sure Boy’ na Mudathir Yahaya kwa muda usiojulikana, Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limeiagiza timu hiyo kutoa adhabu ya muda maalum.

Wachezaji hao walisimamishwa hivi karibuni na timu hiyo kwa muda usiojulikana kutokana na kosa la utovu wa nidhamu.

Chanzo chetu kutoka Azam FC, kimesema kuwa, TFF imeingilia sakata hilo na kuwataka Azam kutoa adhabu ya muda maalum kwa wachezaji hao ili waweze kurejea kwenye majukumu yao ya kawaida na kama hawataki basi wawaruhusu kwenda kutumikia timu zingine na si kuua vipaji vyao.

“Ni kweli TFF imewataka viongozi wa Azam kutoa adhabu maalumu kwa wachezaji hao na kama hawawahitaji basi ni vyema wawafukuze ili wakatafute sehemu nyingine ya kucheza endapo kama bado wana malengo nao basi wawape adhabu ya muda maalumu.”

Alipotafutwa Meneja Mwajiri wa Azam FC, Khamis Ally ili azungumzie ishu hiyo ambapo amesema:

“Nilikutana na viongozi wa TFF wakati nikielekea Zanzibar kwenye shughuli zangu za kazi wakaniambia wamenitumia barua nikirejea Dar es Salaam nitaisoma ili tuweze kuwajibu.”

Aidha Championi lilimtafuta Mwenyekiti wa Chama cha Wanamichezo nchini, (SPUTANZA), Mussa Kisoki ili azungumzie pia sakata hili amesema:

“Siyo sisi tuliotuma hiyo barua Azam ila ni TFF wenyewe maana hata kwenye kanuni zetu jambo hilo lipo kwa kuwa huwezi kumpa adhabu mchezaji isiyoeleweka lini mwisho wake ila nimefurahia kuona wachezaji husika wakienda kuwashitaki TFF maana ni haki yao hata kama wamekosea.

Chanzo: globalpublishers.co.tz