Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Simba, Nabi amvaa Aucho

Aucho Bangala Inonga Kisa Simba, Nabi amvaa Aucho

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa hakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na viungo wa timu hiyo akiwemo Khalid Aucho katika mchezo wao dhidi ya Simba hali iliyomlazimu kukaa nao chini ya kuwapa program mpya kabla ya kuwavaa Rivers United katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nabi ametoa kauli hiyo kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha kilichoonyeshwa na safu yake ya kiungo katika mchezo dhidi ya Simba ambao ulipelekea kupoteza kwa mabao 2-0 tofauti na malengo yake.

Yanga imeanza maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Rivers United unaotarajia kupigwa Aprili 23, mwaka huu nchini Nigeria katika mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Nabi alisema kuwa hakupendezwa na namna safu yake ya kiungo ilivyocheza katika mchezo huo hali iliyopelekea kulazimika kuwapa program mpya kabla ya mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Rivers.

“Binafsi hatukuwa na wakati mzuri katika safu ya kiungo kutokana na namna ambavyo walikuwa chini sana tofauti na nyakati nyingine hali iliyosababisha matokeo mabaya upande wetu.

“Hii imenifanya tuweke mikakati na program mpya ambazo pia zitahusisha washambuliaji kuelekea kwenye mchezo wetu ujao.

“Najua tuna mchezo mgumu sana mbele yetu dhidi ya Rivers kwa sababu malengo yetu ni kuona tunapata matokeo mazuri na kurejea katika hali yetu ya siku zote kwa kuhakikisha kila mchezaji anatambua majukumu yake na anaweza kuyatimiza maana tunachokiangalia ni uwezekano wa kushinda ugenini,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: