Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Ronaldo, Al Nassr yavuna mamilioni ya wafuasi

Ronaldo Al Nassr Ks.jpeg Cristiano Ronaldo

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, Cristiano Ronaldo kuhamia klabu ya Al Nassr FC ya Saudi Arabia klabu hiyo imefurika wafuasi kutokana na umaarufu wa chapa ya CR7.

Klabu hiyo sasa ina wafuasi wengi kwenye ukurasa wa Instagram kuliko vilabu vyote vya Ligi kuu England nje ya vilabu vilivyozoeleka kuwa ndani ya sita bora (top 6).

Kabla ya ujio wa Ronaldo Al Nassr FC ilikuwa na wafuasi takribani 860,000 lakini mpaka sasa ukurasa wa klabu hiyo umegonga wafuasi (followers) milioni 10.1 (10,100,000) zaidi ya vilabu vyote EPL mbali na Arsenal, Liverpool, Manchester City, Manchester United, Chelsea na Tottenham.

Sio mara ya kwanza kwa Cristiano Ronaldo kufanya hivyo, ikumbukwe hali kama hii ilitokea wakati Mreno huyo alipohamia Juventus kutoka Real Madrid mnamo 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live