Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Raja, mabosi Simba wawaweka kitimoto Baleke, Chama

Baleke Chama Er Kisa Raja, mabosi Simba wawaweka kitimoto Baleke, Chama

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba umefanya kikao na wachezaji wao juzi mara baada ya kurejea nchini Guinea ambao wameahidi kuwapa ushindi dhidi ya Raja Casablanca ya nchini Morocco.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kesho Jumamosi saa moja kamili usiku kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ilirejea kutoka Guinea ambako ilikwenda kucheza dhidi ya Horoya AC mchezo uliomalizika kwa Simba kufungwa bao 1-0.

Akizungumza nasi, Mwenyekiti wa timu hiyo, Murtaza Mangungu alisema kuwa uongozi ulifanya kikao na wachezaji wote kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao.

Mangungu alisema kuwa wachezaji hao wameahidi kupambana kwa dakika 90 kuhakikisha wanapata ushindi ili kurejesha morali kuelekea mchezo unaofutia wa kimataifa.

Aliongeza kuwa ushindi wa mchezo huo utaongeza hali ya kujiamini na kufanya vema katika michezo mingine ijayo ili wafanikishe malengo yao kufuzu Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Mchezo wetu dhidi ya Raja Casablanca wa hapa nyumbani, ndio utatupa mwanga halisi ya hatima yetu hivyo ni lazima tushinde tufanikishe malengo yetu baada ya kutoka kufungwa dhidi ya Horoya.

“Hivyo viongozi tulizungumza na wachezaji na benchi la ufundi kuelekea mchezo huo na kutuambia kuwa wapo tayari kutupa ushindi wa kwanza hapa nyumbani kwetu.

“Kikubwa mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuwasapoti wachezaji wetu, na dhumuni letu kuona uwanja unajaa siku hiyo,” alisema Mangungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live