Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Kichapo, Ronaldo avunja simu ya Shabiki

Ronaldo Broke Manchester United walikubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Everton

Sun, 10 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi wa Merseyside wamethibitisha kuwa wanafuatilia taarifa ya tukio ambalo Cristiano Ronaldo wa Manchester United anatuhumiwa kwa kuikwapua simu ya shabiki wa Everton na kuivunja.

Tukio hilo inadaiwa lilitokea jana Aprili 9, 2022 baada ya Man United kufungwa bao 1-0 na Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park katika Premier League ambapo Ronaldo aliomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ronaldo amesema anamkaribisha shabiki huyo kutembelea Uwanja wa Old Trafford wakati wowote United itakapokuwa inacheza. Shabiki huyo alikuwa akimpiga picha Mreno huyo wakati akirejea vyumbani baada ya mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live