Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Glazers, mashabiki Utd waunga mkono Bayern

GLLL Kisa Glazers, mashabiki Utd waunga mkono Bayern

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Manchester United, wamewapigia makofi mashabiki wa Bayern Munich walioingia uwanja wa Old Trafford wakiwa wamebeba mabango ya kuwapinga wamiliki wa klabu yao familia ya Glazers.

Tukio hilo limetokea katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Ulaya uliyochezwa Jumanne usiku.

United iliweka rekodi mbovu katika historia ya klabu hiyo kufuatia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya miamba hiyo ya Bundesliga, hata hivyo mashabiki wa Bayern walionyesha sapoti kubwa dhidi ya wapinzani wao.

Man United ilitambua kuwa ushindi ndo ungewaweka salama kama inataka kusonga mbele raundi ya 16 bora, lakini winga wa Bayern, Kingsley Coman akatibua mipango kwa kuifungia timu yake bao na kuindosha moja kwa moja.

Lakini licha ya kichapo hicho kuna matukio ya kuvutia yalitokea wakati mechi inaendelea ikihusisha mashabiki wa timu hizo mbili kutokana na historia zao.

Kabla ya mtanange huo, mashabiki wa Bayern walibeba mabango ya kupinga gharama kubwa za tiketi ambazo zilipanda kwa asilimia kubwa Old Trafford. Bango la kwanza limeandikwa "Pauni 50 milioni Glazers mmeua." bango lingine likaandika "20 ni nyingi."

Haikuchukua muda mashabiki wa Man United wakawapigia makofi mashabiki wa Bayern kutokana na sapoti yao kubwa waliyoonyesha, kisha wakaanza kuimba nyimbo za kuwadhihaki Glazers.

Mashabiki wa Man United, wamewadhihaki wamiliki wao kwa muda mrefu kutokana na uongozi mbovu ambao haujaleta mafaniki ndani ya klabu hiyo, huku mmiliki mpya Sir Jim Ratcliffe akitarajiwa kununua hisa kwa asilimia 25.

Bosi huyo wa kampuni ya INEOS atakuwa akisimamia masuala yote ya michezo endapo atafanikiwa kununua hisa hizo, hata hivyo mashabiki hawakupendekezwa na mpango huo.

Wakati huo huo, mashabiki wa Man United waliibuka mtandaoni kuipongeza Bayern kutokana na sapoti yao kubwa.

Shabiki mmoja akaandika:"Mashabiki wa Bayern wako vizuri. Tunawaheshimu sana." Shabiki mwingine akasema: "Naipenda Bayern, klabu ya kipekee." Shabiki wa tatu akamalizia kwa kusema: "Natumaini watabeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu."

Akizungumza baada ya kutolewa Ligi Mabingwa Ulaya kocha Erik ten Hag alisema: " Hatukupoteza mechi, huo ndo ukweli. Tulionyesha kiwango bora lakini pia tulifanya makosa, makosa binafsi yametugharimu, mwisho wa siku haikutosha kwa upande wetu, kiwango chetu kilikuwa kizuri hatukustahili kufungwa, lakini tumefungwa, timu imefanya kazi vizuri, safu ya ulinzi ilikuwa nzuri, walishambulia lakini hatukutumia nafasi vizuri."

Man United imeshindwa kupata ushindi katika mechi nne kati ya sita hatua ya makundi, pia imeweka rekodi mbovu ya kuruhusu mabao 15 kwenye michuano hiyo msimu huu.

Msimu huu hakuna timu za England zilizoshiriki hatua ya makundi zilizoruhusu mabao mengi zaidi ya Mashetani Wekundu.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Copenhagen ilifanikiwa kutinga raundi ya 16 bora na kuungana na Bayern baada ya kuifunga Galatasaray bao 1-0.

Chanzo: Mwanaspoti