Benchi la ufundi la Yanga limesema limefanya mabadiliko ya mfumo wake wa kiuchezi katika mechi za hivi karibuni ili kuruhusu kucheza na mastraika wawili jambo ambalo halijazoeleka katika kikosi hicho.
Hayo yamesemwa na Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze wakati akijibu swali kuhusu kikosi hicho kupata matokeo kiduchu katika mechi zao za hivi karibuni.
"Katika mechi hizi mbili tumekuwa tukijaribu kuingiza mfumo mpya wa kucheza na washambuliaji wawili ndio maana imekuwa ikileta changamoto kidogo ya ufungaji.
"Tutarejea kwenye viwanja vya mazoezi kuboresha, lakini pia kuna baadhi ya Wachezaji walikosekana, Feisal, Aucho, Morrison, Aziz Ki, Bangala, ndio maana tuka-struggle kufunga. Tunaamini kwenye michezo ijayo baadhi yao watarejea.
"Lakini kitu kikubwa zaidi kwetu kuliko vyote tunavyozingatia ni kupata points (3)," Cedric Kaze akitafsiri maneno aliyosema kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi.