Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Branthwaite, Man United yageukia watatu

Whiteee Kisa Branthwaite, Man United yageukia watatu

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imewaweka kwenye rada mabeki watatu ambao inafikiria kuwasajili ikiwa Everton itaendelea kushikilia msimamo wao wa kutaka Pauni 70 milioni kwa ajili ya kumuuza Jarrad Branthwaite katika dirisha hili.

Awali Man United iliwasilisha ofa inayofikia Pauni 35 milioni ambayo ilikataliwa na wakaambiwa watoe Pauni 70 milioni, ambayo inaona ni kubwa sana na sasa inapambana kuwashawishi mabosi wa Everton wakubali kumuuza.

Ikiwa watakataa Man United, inafikiria kuwasajili mabeki wengine ikiwa pamoja na Marc Guehi kutoka Crystal Palacem, Leny Yoro wa Lille na Jean-Clair Todibo kutoka Nice.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinaeleza Everton wana mpango wa kuendelea kusalia na fundi huyu kwa msimu ujao.

Man United inataka kuboresha eneo lao la ulinzi lakini hawataki kutumia kiasi kikubwa sana cha pesa kwa sababu bado inahitaji kuweka sawa maeneo mengine ili kufanya vizuri zaidi kwa msimu ujao na itashiriki michuano ya Ulaya ya Kombe la Europa League hivyo inataka kujipanga vizuri.

Chanzo: Mwanaspoti