Kikosi cha Biashara United ya Mara, maarufu kama wanajeshi wa mpakani, wameutangazia Umma wa wapenda soka kuahirishwa kwa mchezo wao wa Oktoba 19 dhidi ya Tanzania Prisons.
Biashara ambayo ilipaswa kusafiri kuelekea Sumbawanga, imearifu kuwa mechi hiyo itapigwa Oktoba 27, katika uwanja ule ule wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Biashara United kwa sasa inajiandaa na mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Klabu ya Al Ahly Tripoli kutoka nchini Libya.
Mchezo huo utapigwa Oktoba 23, nchini Libya na hata kuahirishwa kwa mchezo wake na Prisons sababu zinatajwa ni kujiandaa na mechi hiyo.
Katika mchezo uliopigwa mwishoni mwa juma katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, biashara iliibuka na ushindi wa magoli 2-0.