Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipute cha Premier baada ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Zdc Epl Kipute cha Premier baada ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Ratiba ya Ligi Kuu England msimu wa 2024/2025, imeshatoka huku ikionyesha kuwa kipute hicho kinatarajiwa kuanza Agosti 16, 2024 ambapo timu zote zitacheza wikiendi ya kwanza ya ufunguzi wa michuano hiyo.

Pamoja na ligi hiyo kusubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka EPL lakini mwezi mmoja baada ya kuanza itaanza na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo inasubiriwa kwa nguvu kubwa.

England inawakilishwa na Aston Villa ambao ni wageni kwenye michuano hii, Arsenal, Manchester City na Liverpool.

Hata hivyo, mfumo wa Ligi ya Mabingwa kwa sasa umebadilika baada ya timu kuongezeka, chini ni mechi ambazo timu za England zitarudi nyumbani kucheza siku mbili baada ya kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal inaonekana kuwa na mzigo mzito zaidi kwani mchezo wake wa kwanza tu baada ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya itakutana na Manchester City ambayo nayo itakuwa imetoka kwenye michuano hiyo lakini pia watakutana baada ya mchezo wa mwisho.

Mechi za Aston Villa baada ya kutoka kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa

Septemba 21: Wolves (nyumbani)

Okt 5: Man Utd (nyumbani)

Okt 26: Bournemouth (nyumbani)

Nov 9: Liverpool (ugenini)

Nov 30: Chelsea (ugenini)

Des 14: Nottingham Forest (ugenini)

Jan 25: West Ham (nyumbani)

Feb 1: Wolves (ugenini)

Mechi za Liverpool

Sept 21: Bournemouth (nyumbani)

Okt 5: Crystal Palace (ugenini)

Okt 26: Arsenal (ugenini)

Nov 9: Aston Villa (nyumbani)

Nov 30: Manchester City (nyumbani)

Des 14: Fulham (nyumbani)

Jan 25: Ipswich Town (nyumbani)

Feb 1: Bournemouth (ugenini)

Mechi za Arsenal

Sept 21: Man City (ugenini)

Okt 5: Southampton (nyumbani)

Okt 26: Liverpool (nyumbani)

Nov 9: Chelsea (ugenini)

Nov 30: West Ham (ugenini)

Des 14: Everton (nyumbani)

Jan 25: Wolves (ugenini)

Feb 1: Man City (nyumbani)

Mechi za Man City

Sept 21: Arsenal (nyumbani)

Okt 19: Wolves (ugenini)

Okt 26: Southampton (nyumbani)

Nov 9: Brighton (ugenini)

Nov 30: Liverpool (ugenini)

Des 14: Man Utd (nyumbani)

Jan 25: Chelsea (nyumbani)

Feb 1: Arsenal (ugenini)

Chanzo: Mwananchi