Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipre Jr injini ya Azam Fc inayozitoa udenda Simba, Yanga

Kipre Jr Jr Kipre Jr injini ya Azam Fc inayozivutia Simba, Yanga mezani

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Azam FC ni miongoni mwa timu zenye wachezaji wengi wenye viwango vikubwa na wasifu wao umeshiba. Kwa haraka haraka utawataja, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yanick Bangala kutokana na kucheza kwao Yanga, timu yenye mashabiki wengi nchini lakini wapo wengine wengi. Miongoni mwao ni winga hatari Muivory Coast, Kipre Jr (24). Jina lake kamili ni Kipre Tiagori Emmanuel Junior lakini hufupishwa na kuitwa Kipre Junior.

Azam FC ni miongoni mwa timu zenye wachezaji wengi wenye viwango vikubwa na wasifu wao umeshiba. Kwa haraka haraka utawataja, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yanick Bangala kutokana na kucheza kwao Yanga, timu yenye mashabiki wengi nchini lakini wapo wengine wengi. Miongoni mwao ni winga hatari Muivory Coast, Kipre Jr (24). Jina lake kamili ni Kipre Tiagori Emmanuel Junior lakini hufupishwa na kuitwa Kipre Junior. Staa huyo alijiunga na Azam mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Sol FC ya nchini kwao Ivory Coast na kutambulishwa na bosi wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa. Alianza msimu kwa kasi, lakini wengi walimuona machachari kuliko hatari na msimu huu ni kama ameamua kuwajibu kwa kuonyesha balaa lake akiwa ndani ya jezi ya Azam. Mwanaspoti kupitia makala haya linakuletea uchambuzi wa Kipre JR namba anavyoibeba Azam msimu huu. DAKIKA 1163 Kipre ni miongoni mwa wachezaji wa Ligi Kuu msimu huu waliocheza dakika nyingi hadi sasa. Staa huyo amecheza mechi 19 kati ya 21 ilizocheza Azam hadi sasa. Ni mechi mbili tu ambazo hajacheza ambayo ni ile ya kwanza ya ligi dhidi ya Tabora United iliyopigwa kwa dakika 15 tu na Azam kushinda 4-0. hata hivyo alikuwa benchi huenda angeingia kama mechi ingechezwa kwa dakika zote 90. Mechi hiyo iliisha muda huo kwakuwa Tabora iliingia uwanjani ikiwa pungufu. Waliingia wachezaji wanane tu na baadae wachezaji wawili wakaumia na kushindwa kuendelea na mechi hivyo mchezo ukaisha kutokana na Tabora kutokuwa na wachezaji walau saba uwanjani kama kanuni inavyotaka. Mechi nyingine ni ile ya mzunguko wa kwanza Ambapo Azam ilicheza na Singida Fountain Gate na kushinda 2-1, hiyo Kipre hakuwepo lakini nyingine zote ilizocheza Azam msimu huu ameugusa mpira. Ukijumlisha dakika zote alizocheza kwenye mechi hizo 19, hesabu inakuja amecheza dakika 1163. Hiyo inaonesha dhahiri ni namna gani ni tegemeo na njini ya kikosi cha Azam ambacho mara nyingi hufanyiwa mabadiliko ‘Rotations’. AWAFUNIKA PACOME, NZENGELI Ukiangalia msimamo utaikuta Azam ni timu ya pili kwenye msimamo wa ligi lakini pia ni ya pili kwenye kufunga mabao ikipachika 47, mawili nyuma ya vinara Yanga waliofunga 49. Baada Feisal aliyehusika kwenye mabao 18, kati ya 47 ya Azam hadi sasa anayefuata ni Kipre aliyehusika katika mabao 14 akifunga sita na kutoa asisti nane katika mechi 19 alizoichezea timu hiyo. Hizo ni namba nzuri kwa winga hususani wa ligi yenye ushindani mkubwa kama ilivyo Ligi Kuu. Hakuna winga aliyehusika kwenye idadi hiyo ya maba hadi sasa, wanaofuata ni Pacome Zouzoua wa Yanga aliyehusika kwenye mabao 10 akifunga saba na kutoa asisti nne sawa na Maxi Nzengeli akiyefunga nane na kuasisti mara mbili. MKALI WA ASISTI Ukichungulia orodha ya wanaoongoza kwa kutoa pasi za mwisho ‘assist’ utamkuta amekaa kileleni na asisti zake nane. Anayemfuatia ni beki Kouassi Attohoula Yao na kiungo Stephene Aziz Ki wa Yanga ambao kila mmoja ameasisti mara saba. Wengine ni Impiri Mbombo wa Tabora United, Rahim Shomari na Awesu Awesu wa KMC, Fei Toto, na Clatous Chama wa Simba kila mmoja akiwa na asisti tano. SIMBA, YANGA MEZANI Kama ulikuwa hujui sasa unatakiwa kujua kuwa vigogo wa soka nchi Simba na Yanga zinammezea mate winga huyo tangu ametua Azam na ziko tayari kumsajili muda wowote ambapo Azam itakubali kumuuza. Yanga ilienda mbali zaidi na kutuma ofa Azam ya kutaka kumsajili ambapo ilifanya hivyo Desemba 28, 2022 ikiomba kukaa mezani kujadili namna ya kumpata Kipre na kiungo James Akaminko ambao Azam iligoma kuwauza Jangwani. Ukiachana na Yanga, Simba nayo iliwahi kugonga mlango ya Azam ikimtaka winga huyo lakini matajiri wa Azam wakaweka ngumu ila Mwanaspoti linajua bado wanamsimbazi wanammendea kimya kimya. Huyo ndiye Kipre Tiagori Emmanuel Junior, Staa anayevaa jezi namba 10 ya matajiri wa Chamazi, Azam FC.

Chanzo: Mwanaspoti