Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipre Jr atupia mbili, Azam ikiiua Namungo

Kipre Azam Fc Kipre Jr atupia mbili, Azam ikiiua Namungo

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mabao mawili ya kipindi cha pili kutoka kwa Kiungo mshambuliaji, Kipre Junior yameiwezesha Azam FC usiku wa jana kuiua Namungo ikiwa ugenini katika mechi kali ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi.

Ushindi huo ulioifanya Azam kuzidi kuibana Yanga iliyopo kileleni kwa kufikisha pointi 50, tano pungufu na ilizonazo watetezi hao wa Ligi Kuu wenye pointi 55. Hata hivyo, Azam imecheza mechi 22, wakati Yanga imecheza michezo 21 hadi sasa.

Katika mchezo huo wa jana, wenyeji Namungo waliibana Azam katika kipindi cha kwanza, licha ya kuwepo kosa kosa nyingi na kufanya dakika 45 za kwanza ziishe bila timu hizo kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kuongeza mashambulizi makali, lakini ni wageni walinufaika kwa kuandika bao la kwanza dakika ya 62 kupitia Kipre Jr.

Wakati Namungo ikitafuta namna yabkurudisha bao hilo, Kipre alitumia jingine la pili dakika ya 84 baada ya kuipangua ngome ya wenyeji na kutupia nyavuni na kumfanya afikishe mabao tisa hadi sasa katika ligi hiyo.

Ushindi huo umeifanya Azam kulipa kisasi cha kufungwa na Namungo katika mechi ya duru la kwanza ilipofungwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa nyumbani wa Azam Complex.

Mechi hiyo ilipigwa Oktoba 27 mwaka jana, siku chache baada ya Azam kufumuliwa mabao 3-2 na Yanga.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumanne, kwa mechi mbili, saa 10 jioni Mtibwa Sugar inayoburuza mkia itaialika KMC kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani Morogoro na saa 1 usiku itakuwa zamu ya Dodoma Jiji kuikaribisha JKT Tanzania huku zote zikitoka kupata sare katika mechi zilizopigwa jana Jumamosi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: